SYRIA-UN-WATOTO-USALAMA

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hali ya watoto Syria

Mashirika ya haki za watoto nchini Syria yameonya kuwa vita nchini humo vimesababisha kuharibu watoto kimwili na kisaikolojia.
Mashirika ya haki za watoto nchini Syria yameonya kuwa vita nchini humo vimesababisha kuharibu watoto kimwili na kisaikolojia. REUTERS/Sultan Kitaz

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa watoto wanaosububiriwa kuokolewa nchini Syria na kupelekwa katika maeneo salama, wanatumiwa kama kigezo cha serikali na waasi kufikia matakwa yao.

Matangazo ya kibiashara

Watoto wamekwama katika ngome ya upinzani jijini Damascus na wanahitaji msaada wa haraka wa huduma ya afya na chakula.

Tayari watoto 12 wameshaondolewa na wengine 13 wanatarajwia kuondolewa hivi leo.

Mashirika ya haki za watoto nchini Syria yameonya kuwa vita nchini humo vimesababisha kuharibu watoto kimwili na kisaikolojia.

Wakimbizi watoto walio katika ya umri wa kwenda shule ambao wamekimbilia katika nchi jirani wameendelea kukosa elimu na wanalazimika kufanyakazi ili kujikimu.

Zaidi ya nusu ya wakimbizi wa Syria milioni 2.2 ni watoto, wengi wakikabiliwa na hatari kubwa na hata nje ya eneo la vita.

Hatari hizo ni pamoja na athari za kimwili na kisaikolojia, na baadhi wamepotza maisha.