SYRIA-USALAMA

Mapigano makali yaendelea kurindima Harasta, kaskazini mwa Damascus

Askari wa Syria katikamkoa wa Damascus (picha ya zamani).
Askari wa Syria katikamkoa wa Damascus (picha ya zamani). AFP

Mapigano makali yanaendelea katika Ghuta ya mashariki , kaskazini mwa Damascus, ambapo jeshi la Syria, likisaidiwa na jeshi la anga la Urusi, linajaribu kuvunja makao makuu ya kambi ya vikosi vya serikali katika mji wa Harasta, iliyoshikiliwa wiki iliyopita na waasi. Mapigano yameua watu kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Waasi walivamia na kudhibiti sehemu ya kambi ya Harasta, kaskazini mwa Damascus, ambapo askari 200 wamezingirwa kwa miezi mitatu sasa. Hatua hii imeyawezesha makundi ya waasi kukaribia katikati ya mji mkuu wa Syria, na hivyo serikali kuchukua uamuzi wa kutuma askari wengi, ikiwa ni pamoja na vitengo vya kikosi cha ulinzi wa rais.

Siku ya Jumatano majeshi ya serikali yalizindua mashambulizi kabambe ili kujaribu kurejesha kwenye himaya yao eneo linalodhibitiwa na waasi. Waasi walijibu kwa kuelekea makao makuu ya manispaa. Mapigano yanaendelea, huku ndehe za kivita za Urusi zikiendesha mashambulizi makubwa ya angani ili kujaribu kuwarejesha nyuma waasi na kuvunja njia wanazotumia kwa kupata silaha na chakula.

Harasta ni eneo muhimu, kwani inaunganisha barabara kuu ya Damascus kuelekea Homs.

Lakini mapigano hayajawahi kusimama katika eneo hili kubwa linaloanzia kaskazini hadi mashariki mwa mji mkuu wa Syria. Waasi wanaopigana katika mji wa Harasta ni kutoka kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Ahrar al-Sham.