SYRIA-USALAMA

Watu 28 wauawa katika mashambulizi ya angani Syria

Ndege ya kivita aina ya Su-24M ya Urusi ikitua katika kambi ya Hmeimim.
Ndege ya kivita aina ya Su-24M ya Urusi ikitua katika kambi ya Hmeimim. REUTERS/Ministry of Defence of the Russian Federation

Watu 28 wamepoteza maisha katika ngome ta waasi wa upinzani nchini Syria jijini Damascus, baada ya mashabulizi ya angaa yaliyotekeleza na ndege za kivita za Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Waangalizi wa mzozo wa Syria na watetezi wa Haki za Binadamu nchini humo wanasema kuwa, shambulizi hilo lilitokea katika mtaa wa Misraba.

Watoto saba na wanawake 11 ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha kwa mujibu wa Mashirika hayo ya kutetea haki za binadamu.

Inaelezwa kuwa idadi iliongezeka kwa sababu watalaam wa afya walishindwa kuondoa kifusi cha majengo yaliyokuwa yamewaangukia raia hao wa kawaida.

Mashariki mwa jiji la Damscus, ndio ngome ya waasi wa upinzani wanaosalia baada ya Urusi kuisaidia Syria kuwashinda waasi hao katika maeneo mengi katika jiji hilo.

Mapigano nchini Syria yameababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kubaki bila mahitaji muhimu kama chakula, dawa na maji.

Serikali ya Syria imeendelea kukanusha kuwalenga raia wasiokuwa na hatua katika mashambulizi hayo.