SYRIA-USALAMA-SIASA

Watu 23 waangamia katika mashambulizi ya angani Ghouta, Syria

Majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya angani katika eneo lililozingirwa la Ghouta mashariki, Januari 9, 2018.
Majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya angani katika eneo lililozingirwa la Ghouta mashariki, Januari 9, 2018. REUTERS/Bassam Khabieh

Mashambulizi ya angani katika Ghouta ya mashariki, eneo linaloshikiliwa na waasi nje ya mji wa Damascus, yameua watu23, shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) limesema leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yameathiri maeneo ya Zamalka, Arbain, Hazza na Beitou Soua, limesema shirika la haki za Binadamu la OSDH, lenye makao yake makuu London, nchini Uingereza.

Ghouta ya mashariki, ngome ya mwisho ya jeshi la Syria ambayo bado inashikiliwa na waasiimezingirwa kwa miakakisaidiwa na ndege za kijeshi za Urusi na wanamgambo wa Kishia.

Wakati huo huo mwanamke mmoja ameuawa na watu watatu wamejeruhiwa na katika mashambulizi ya mabomu yaliyorushwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, unaoshikiliwa na majeshi ya serikali, shirika la habari la Sana limearifu.

Mji wa zamani wa Damascus, ambao unashikiliwa na majeshi ya serikali, uko karibu na eneo la waasi ambapo Ghouta ni sehemu yake.