SYRIA-MAREKANI-URUSI-UN-USALAMA

Marekani na Urusi watupiana vijembe kwenye Umoja wa Mataifa

Mabalozi wa Urusi Vassily Nebenzia (kwa mgongo) na balozi wa Marekani Nikki Haley wanazungumza katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 5 Februari 2018.
Mabalozi wa Urusi Vassily Nebenzia (kwa mgongo) na balozi wa Marekani Nikki Haley wanazungumza katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 5 Februari 2018. Drew Angerer/Getty Images/AFP

Watu wasiopungua 29 wanaripotiwa kupoteza maisha siku ya Jumatatu (Februari 5) wakati wa mashambulizi ya angani yaliyoendeshwa na majeshi ya serikali katika eneo linaloshikiliwa na waasi karibu na Damascus.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria lenye makao yake makuu London, nchini Uingereza, watu tisa wameathirika na matatizo ya kupumua, na hivyo kushuku kwamba katika mashambulizi hayo jeshi la Syria lilitumia gesi ya kemikali. Taarifa ambayo mashirika mbalimbali ya kitibabu yamethibitisha. Suala hilo lilizua mjadala mkubwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mashambulizi hayo yaliendeshwa siku ya Jumatatu katika jimbo la Goutha ya mashariki, hasa kaika maeneo ya Zamalka, Arbain, Hazza na Beit Sawa. Hii ni moja ya ngome zinazoshikiliwa na waasi wa Syria. Ndege za kivita pamoja na majeshi ya nchi kavu, waliendesha mashambulizi ya angani, mashambulizi ambayo yaliua watu wasiopungua 29, ikiwa ni pamoja na 10 katika eneo pekee la Beit Sawa, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH).

Waasi waljibu, wakirusha makombora katika mji mkuu Damascus, hali ambayo ilisababisha kifo cha mwanamke mmoja na wengine zaidi ya kumi na tano kujeruhiwa kwa mujibu wa shirika la habari la Sana.

OSDH pia imeelezea kutokea visa vya magonjwa mbalimbali, matatizo ya kupumuakutokana na matumizi ya zilaha za kemikali. Siku ya Jumapili, Washington na OSDH walidai kuwa jeshi la Syria lilitumia silaha za kemikali wakati wa mashambulizi ya angani katika mkoa wa Idleb, unaoshikiliwa na waasi kaskazini magharibi mwa Syria.

Kutokana na hali hiyo Marekani na Urusi walishambuliana kwa maneno makali katika kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.

Marekani iliishtumu Urusi kuchelewesha kupitishwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalolaani mashambulizi ya kemikali ya hivi karibuni nchini Syria.

Urusi, kwa upande wake, ilijitetea, ikidai kuwa ni "kampeni ya propaganda" yenye lengo la "kuishtumu serikali ya Syria" kwa mashambulizi ambayo "wahalifu hawajulikani".