URUSI-MAREKANi-UTURUKI-SYRIA-USALAMA

Urusi yalaani mashambulizi dhidi ya washirika wa Uturuki Syria

Vikosi vya Uturuki na wapiganaji wa kundi la waasi linalosaidi serikali ya Damascus wakishikilia bendera kwenye Mlima Baalaaya, kaskazini mashariki mwa Afrin, tarehe 28 Januari 2018.
Vikosi vya Uturuki na wapiganaji wa kundi la waasi linalosaidi serikali ya Damascus wakishikilia bendera kwenye Mlima Baalaaya, kaskazini mashariki mwa Afrin, tarehe 28 Januari 2018. REUTERS/ Khalil Ashawi

Balozi wa Urusi kwenye umoja wa Mataifa amekashifu vikali mashambulizi yaliyofanywa na Marekani kuwalenga wapiganaji wanaoisaidia Serikali ya Damascus katika vita dhidi ya kundi la Islamic State kwenye jimbo la Deir Ezzor na kuua wapiganaji zaidi ya 100.

Matangazo ya kibiashara

Balozi Vasilly Nebenzia amesema nchi yake imechukizwa na mashambulizi ya Marekani na kusema kilichofanyika ni uhalifu wa kivita huku akikosoa pia makundi ya wapiganaji wasiotaka kufikia makubaliano.

Kwa upande wake nchi ya Marekani kupitia kwa msemaji wa Pentagon Dana White, anasema kilichofanywa na nchi yake ni kujilinda dhidi ya hatari ambayo vikosi vyake vilikuwa vikikabiliwa nayo.

Nchi ya Urusi katika kujibu kilichofanywa na Marekani imeshambulia kwenye maeneo yanayokaliwa na wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani hatua ambayo inafanya mzozo wa Syria kuwa mgumu zaidi katika kuupatia suluhu.