SYRIA-IS-USALAMA

Wapiganaji hatari wa IS wakamatwa Syria

Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh wanahusishwa pia kuwa wanachama wa kundi la kigaidi nchini Uingereza linalofahamika kama 'Jihadi John'.
Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh wanahusishwa pia kuwa wanachama wa kundi la kigaidi nchini Uingereza linalofahamika kama 'Jihadi John'. Reuters

Wapiganaji wawili wa Islamic State raia wa Uingereza ambao walionekana katika mikanda ya video ikionesha wakiwakata shingo mateka, wamekamatwa nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka Wizara ya Ulinzi nchini Marekani imethibitisha kukamtwa kwa magaidi hao, na kuwataja kuwa Alexanda Kotey na El Shafee el-Sheikh.

Alexanda Kotey, mwenye umri wa miaka 34, na El Shafee Elsheikh, mwenye miaka 29, ni miongoni mwa vijana wawili waliokuwa wanasakwa kati ya wenzao ambao walikwisha kamatwa.

Kundi hili la vijana wanne kutoka Uingereza katika kundi la IS walikuwa ni kundi hatari linalofahamika kama Beatles, kutokana na lafudhi yao wanapozungumza.

Kundi hilo lililokuwa likihusika na utoaji mateso pamoja na kuua katika kundi la Islamic State (IS) linadaiwa kuwachinja zaidi ya watu 27 mateka kutoka nchi za kimagharibi.

Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh wanahusishwa pia kuwa wanachama wa kundi la kigaidi nchini Uingereza linalofahamika kama 'Jihadi John', lakini pia imeelezwa wamekuwa wakihusika katika utekaji nyara wa raia wa kigeni nchini Syria.