SYRIA-UN-VITA

Umoja wa Mataifa kupitisha azimio jipya kuhusu vita nchini Syria

Mapigano katika ngome ya waasi Ghouta Mashariki jijini Damascus watoto wakiokolewa katika eneo la vita
Mapigano katika ngome ya waasi Ghouta Mashariki jijini Damascus watoto wakiokolewa katika eneo la vita REUTERS/ Bassam Khabieh

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupitisha azimio la kusitishwa kwa vita nchini Syria kwa siku 30 kwa lengo la kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia waathiriwa vinavyoendelea.

Matangazo ya kibiashara

Azimio hili linaandaliwa na Sweden na Kuwait, lengo kubwa likiwa ni kumaliza mzozo nchini humo hasa Mashariki mwa mji wa Ghouta, ngome ya upinzani.

Mashambulizi dhidi ya kijeshi dhidi ya wapinzani wa serikali ya Syria, yamesababisha watu 240 kupoteza maisha kwa muda wa siku tano zilizopita.

Mapigano nchini Syria yamesababisha vifo vya maelfu ya watu tangu mwaka 2011 na Mamilioni kukimbilia katika mataifa jirani.

Wiki iliyopita, kulikuwa na juhudi za mazungumzo ya amani nchini Urusi lakini, upinzani ukasusia.

Mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa, hayajazaa matunda yeyote hadi sasa.