MAREKANI-ISRAEL-USHIRIKIANO

Marekani yafutilia mbali hoja ya Israel kuhusu makazi mapya

Wazir Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.
Wazir Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. REUTERS

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa alikuwa na mazungumzo kwa muda mrefu na utawala wa Trump kuhusu kuongezwa kwa makazi katika Ukingo wa Magharibi. Hata hivyo ikulu ya White House imekataa hoja hiyo, hatua ambayo imewashangaza wengi.

Matangazo ya kibiashara

Kuunganishwa kwa makazi ya kiraia ya Israeli katika maeneo ya Palestina yaliyokaliwa kimabavu itavuruga mchakato wa amani na ufumbuzi kwa mataifa haya mawili, yaani kuundwa kwa taifa la Palestina litakalokuwa jirani na Israeli.

Suluhisho hili, ambalo Bw Netanyahu alijitenga nalo baada ya kuingiliwa na kasoro, bado ni kazi kwa sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa.

"Katika suala la matumizi ya uhuru wa Israeli (kwa maeneo tunayokalia), naweza kusema kuwa ni kwa muda mrefu ninaliongelea na Marekani," alisema Netanyahu siku ya Jumatatu mbele ya wabunge kutoka chama chake cha Likud (cha mrengo wa kulia), kulingana na maneno yaliyotolewa na mmoja wa wasemaji wake.

Baadaye kidogo, afisa wa Israeli alitaka kutofautisha maneno ya Waziri Mkuu.

Netanyahu "hajawasilisha mapendekezo maalum ya kuongezwa kwa makazi ya walowezi, kwa hali yoyote, Marekani haijakubaliana na mapendekezo haya," alisema afisa huyo ambaye hakutaja jina lake.

"Israel ilitaka kuijulisha Marekani kuhusu miradi mbalimbali iliyojadiliwa bungeni. Wabunge walisema wazi watafanya kazi ili kuendeleza mpango wa amani wa Rais Trump," ameongeza afisa huyo.

Josh Raffel, msemaji wa ikulu ya White House, amekataa katu katu kufanyika kwa mazungumzo kati ya Marekani na Israeli kuhusu suala hilo.

"Marekani na Israeli hawajawahi kujadili pendekezo hilo na rais anaendelea kujikita na mpango wake wa amani wa kati ya Israeli na Palestina."