IRAN-AJALI-NDEGE

Abiria wote 66 wapoteza maisha baada ya ndege kuanguka Iran

Shirika la ndege la Iran
Shirika la ndege la Iran DR

Abiria wote 66 waliokuwa wanasafiria Shirika la ndege la Aseman wakitokea jiji Tehran kwenda Yasuj nchini Iran wamepoteza maisha baada ya ndege yao kuanguka.

Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo lakini, dalili zinaonesha kuwa hali mbaya ya hewa ilichangia pakubwa.

Maafisa wa uokoaji nao walishindwa kufika kwa wakati katika eneo la tukio kujaribu kuwaokoa baadhi ya abiria.

Ripoti zaidi zinasema kuwa ajali hiyo ilitokea katika mlima Dena, umbali  wa Kilomita 22 kutoka mjini Yasuj.

Iran imekuwa ikikumbana na ajali kama hizi katika miaka ya hivi karibuni.