ISRAEL-IRAN-USALAMA

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aionya Iran

Waziri Mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu akionesha kipande cha ndege ya kijeshi ya Iran iliyoangushwa na wanajeshi wake wiki hii akiwa katika mkutano wa usalama jijini Munich nchini Ujerumani fEBRUARI 18 2018
Waziri Mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu akionesha kipande cha ndege ya kijeshi ya Iran iliyoangushwa na wanajeshi wake wiki hii akiwa katika mkutano wa usalama jijini Munich nchini Ujerumani fEBRUARI 18 2018 ©Lennart Preiss/MSC

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameiambia serikali ya Iran, isiijaribu nchi yake huku akieleza kuwa, ni nchi hatari duniani kiusalama na hatua inastahili kuchukuliwa dhidi yake.

Matangazo ya kibiashara

Netanyahu ametoa kauli hiyo akiwa jijini Munich nhini Ujerumani wakati akihudhuria mkutano wa Kimataifa wa usalama.

Akionesha kipande cha mabaki ya ndege isiyokuwa na rubani iliyoangushwa nchini mwake hivi karibuni ikitokea nchi jirani ta Syria, Netanyahu amesema nchi yake haitaruhusu kushambuliwa na maadui zake.

Aidha, ameonya kuwa Iran inaendelea na mpango wa kutengeza bomu ya kuishambulia Israel, iwapo mkataba wa kusitisha mradi wa nyuklia hautabadilishwa kwa lengo la kuizuia kabisa Tehran kuendelea na mradi huo.

Mkataba huo unaitaka Iran kuachana na mradi huo kwa muda wa miaka kumi.

Wizara ya Mambo ya nje ya Iran imekataa kumjibu Netanyahu, na kupuuza onyo hilo ambalo imesema haiwezi kuzungumzia.