ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Israeli yafanya mashambulizi mapya katika ukanda wa Gaza

Askari wa Israeli karibu na mpaka wa Gaza, Februari 17, 2018.
Askari wa Israeli karibu na mpaka wa Gaza, Februari 17, 2018. REUTERS/Amir Cohen

Ndege za kivita za Israeli zimeendesha mashambulizi mapya mapema leo Jumatatu Alfajiri katika ukanda wa Gaza ambapo ghasia zimeendelea kushuhudiwa.

Matangazo ya kibiashara

Ndege za kivita za Israeli zililenga mitambo ya kijeshi eneo la kusini mwa Palestina linaloongozwa na kundi al Hamas, adui mkuu wa Isarel, jeshi limebaini katika taarifa yake.

Israel inasema ilifanya mashambulizi hayo kama jibu ya kurushwa kwa roketi siku ya Jumapili usiku kutoka upande wa Gaza, ikiwa ni roketi ya pili ndani ya saa 24.

Roketi hiyo ilianguka karibu na Sderot, mji wa Israeli ulio karibu na Palestina, bila kufanya uharibifu, kwa mujibu wa chanzo cha jeshi la Israel.