UTURUKI-SYRIA-USALAMA

Ankara yapuuzia madai ya Syria kuingia Afrin

Askari wa Uturuki kwenye Mlima wa al-Barsaya kaskazini mwa Afrin, Syria.
Askari wa Uturuki kwenye Mlima wa al-Barsaya kaskazini mwa Afrin, Syria. REUTERS/ Khalil Ashawi

Majeshi ya serikali ya Syria hayajaingia katika mji wa Afrin, na hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa wana uwezo wa kufanya hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema leo Jumanne.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Syria ilitangaza siku ya Jumatatu asubuhi kwamba majeshi yake yataingia katika mji huo unaoshikiliwa na wapiganaji wa Kikurdi unaolengwa tangu mwezi Januari na mashambulizi ya jeshi la Uturuki.

Serikali ya Ankara imeonya kuwa jeshi lake halitosita kukabiliana na jeshi la Syria ikiwa litaingia katika mji huo ili kusaidia wanamgambo wa Kikurdi kutoka kundi la YPG.

Serikali ya Kikurdi inawachukulia wapiganaji wa kundi la YPG, mshirika wa chama cha PYD kama tawi la kijeshi la kundi la PKK, ambalo Uturuki unalichukulia kama kundi la kigaidi.