BAHRAIN-HAKI-SIASA

Mwanasiasa maarufu wa upinzani ahukumiwa miaka 5 jela Bahrain

Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Bahraini Nabil Rajab (katikati) akiachiwa huru Februari 11, 2015 huko Manama.
Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Bahraini Nabil Rajab (katikati) akiachiwa huru Februari 11, 2015 huko Manama. AFP

Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Bahraini Nabeel Rajab amehukumiwa leo Jumatano kifungo cha miaka mitano jela kwa kulaani hatua ya muungano wa Kiarabu kuingilia kijeshi katika mgogoro nchini Yemen.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama nchini Bahrein imesema kuwa Nabeel Rajab alitumia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika habari za uongo na kuzeneza uvumi.

Hata hivyo Bw Rajad pia amepatikana na hatia ya kuzagaza habari za uzushi kuhusu visa vya mateso nchini Bahrain, chanzo mahakama na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali wamesema.

Nabeel Rajab, mmoja wa viongozi wa maandamano ya mwaka 2011 yalisababisha kuzuka kwa maandamano makubwa katika mataifa kadhaa ya Kiarabu, aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani mwezi Julai kwa ajili ya "kuzagaza uvumi na habari za uongo" wakati wa mahojiano ya televisheni kwa kuukosoautawala huko Manama.

Hukumu ya leo Jumatanoilitangazwa na Mahakama Kuu ya Jinai ya Bahrain, kimesema chanzo cha mahakama na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali, Bahrain Center for Human Rights (BCHR) na Bahrain Institute for Righta and Democracy (BIRD).

Nabeel Rajab anashtakiwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter "matusi" ambapo alishtumiwa kuikosoa Saudi Arabia na washirika wake, ikiwa ni pamoja Bahrain, kwa kuhusika kwao katika vita vinavyoendelea tangu 2015 nchini Yemen.

Pia alishutumiwa kueneza habari kuhusu visa vya mateso katika jela la Jaw huko Bahrain na "kuitukana" wizara ya mambo ya ndani.

Mwanasiasa huyo wa Upinzani amepatikana na hatia ya "kueneza uvumi na habari za uwongo" na "kuitusi nchi jirani" (Saudi Arabia) , chanzo cha mahakama kimeiliambia shirika la habari la AFP.