SYRIA-UN-USALAMA

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu mashambulizi Ghouta mashariki

Un enfant dans les bras, un homme fuit les bombardements du régime syrien dans la Ghouta orientale, près de Damas, le 19 février 2018.
Un enfant dans les bras, un homme fuit les bombardements du régime syrien dans la Ghouta orientale, près de Damas, le 19 février 2018. ABDULMONAM EASSA / AFP

Umoja wa Mataifa unonya dhidi ya serikali ya Syria kuendelea na mashambulizi Mashariki mwa Ghouta, ngome ya waasi karibu na mji wa Damascus. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa ana "wasiwasi mkubwa" kutokana na kuongezeka kwa machafuko katika eneo hilo siku ya Jumanne, Februari 20.

Matangazo ya kibiashara

Antonio Guterres ametoa wito kwa pande zote kuheshimu kanuni za msingi za haki za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa raia katika vita, msemaji wakeStephane Dujarric amesema.

"Karibu watu 400,000 katika Ghouta mashariki wanakabiliwa na mashambulizi ya angani, " Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameongeza.

Mashambulizi ya angani ya majeshi ya Syria na Urusi dhidi eneo linaloshikiliwa na waasi yaliua watu 106 siku ya Jumanne, kwa mujibu wa Shirika la haki za Binadamu nchini (OSDH).

Siku ya Jumatatu, watu 127waliuawa, kwa mujibu wa shirika hilo. Tangu siku ya Jumapili, Zaidi ya watu 250 wameuawa katika mashambulizi haya ambapo kati ya idadi hiyo 50 wakiwa ni watoto, OSDH imeongeza.