UTURUKI-SYRIA-USALAMA

Uturuki yaonya mtu yeyote kuwasaidia Wakurdi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Kayhan Ozer/Palacio Presidencial

Nchi ya Uturuki inasema yeyote atakayewasaidia wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria, watawashambulia, kauli inayotolewa saa chache baada ya wapiganaji wanaoiunga mkono Serikali ya Damascus kuripotiwa kuingia kwenye mji wa Afrin kuwasaidia wapiganaji hao dhidi ya mashambulizi ya Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

Kitisho hiki cha Uturuki kimetolewa na msemaji wa rais Erdogan, Ibrahim Kalin ambaye amesema kundi lolote litakalowasaidia wapiganaji hao litalengwa na vikosi vyao.

Wakati huohuo mashambulizi yaliyotekelezwa na vikosi vya Serikali kwenye mji wa Ghouta uliko mashariki mwa Syria yamesababisha vifo vya raia zaidi ya 250 hii ni kwa mujibu wa mashirika ya waangalizi.

Katika hatua nyingine nchi ya Ufaransa kupitia Waziri wake wa Mambo ya Kigeni Jean-Yves Le Drian imetaka Umoja wa Mataifa kuhakikisha kunatengwa muda wa usitishwaaji wa mapigano ili kufikisha misaada ya kibinadamu.

Jana Jumanne katibu mkuu wa umoja wa Mataifa ANTONIO GUTTERES alieleza kuguswa na mashambulizi yanayotekelezwa kwenye mji wa Ghouta.