SYRIA-USALAMA

Wapiganaji wa Kikurdi wa YPG waomba msaada kwa jeshi la Syria

Wapiganaji wa kundi la waasi la Free Syrian Army linalosaidiwa na Uturukikaskazini mwa Afrin, Syria, Februari 16, 2018.
Wapiganaji wa kundi la waasi la Free Syrian Army linalosaidiwa na Uturukikaskazini mwa Afrin, Syria, Februari 16, 2018. REUTERS/Khalil Ashawi

Wapiganaji wa Kikurdi wa kundi la YPG waliotumwa Afrin kupambana na askari wa Uturuki kaskazini mwa Syria wameomba msaada wa kijeshi kutoka jeshi la Syria katika hali ya kulinda eneo hilo, msemaji wa kundi hlo amesema.

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji mia kadhaa wanaounga mkono utawala wa Damescus waalitumwa katika uwanja wa vita kupambana dhidi ya majeshi ya Uturuki yanayoendelea na mapigano katika eneo la Afrin, amesema Nouri Mahmoud, msemaji wa Wa Wakurdi.

"Baadhi ya makundi yenye uhusiano na jeshi la Syria yamewasili Afrin lakini si wengi wa kutosha kwa kuweza kuzuia majeshi ya Uturuki kudhibiti eneo la Afrin. Jeshi la Syrialinatakiwa kutimiza wajibu wake wa kulinda mipaka ya Syria," Bw Mahmoud amebainisha.

Wanamgambo wa kundi la YPG, hata hivyo, wamekanusha taarifa kwamba askari wa serikali ya Syria walikuwa wameingia katika maeneo ya Kikurdi ya Aleppo.

Shahidi mmoja aliyenukuliwa na shirika la Haki za Binadamu nchini Syria, OSDH, amesema leo Alhamisi kuwa vikosi vya serikali ya Syria vilikua vimeingia katika maeneo ya Al Halak, Bani Zaid na Bustan al Basha kaskazini mwa Aleppo, maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji wa YPG.