SYRIA-URUSI-USALAMA

Urusi yaagiza usitishwaji wa mapigano Syria

Ghouta mashariki yaendelea kukumbwa na mashambulizi.
Ghouta mashariki yaendelea kukumbwa na mashambulizi. REUTERS/Bassam Khabieh

Rais wa Urusi Vladmir Putin ameagiza vikosi vyake na vile vya serikali ya Syria kusitisha mapigano kwa muda wa saa tano katika mashambulizi yanayofanywa na serikali ya Syria katika maeneo ya mashariki mwa eneo la Ghouta linalodhibitiwa na waasi.

Matangazo ya kibiashara

Jana Jumatatu Marekani iliitolea wito Urusi kuheshimu wito wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kusitisha mapigano katika eneo la Ghouta mashariki, ngome ya waasi, karibu na mji wa Damascus.

Urusi imesema usitishwaji wa mapigano unaanza leo Jumanne na utajumuisha kutengwa kwa kile ilichokiita '' Njia Salama'' kuwawezesha raia kuondoka katika eneo la Ghouta linalokabiliwa na mapigano makali.

Hata hivyo Marekani imeishtumu Urusi kuendelea na mashambulizi katika eneo la Ghouta mashariki na kuishtumu pia kuendelea kuchochea vita nchini Syria,

Hivi karibuni Urusi ilistumu Marekani na Saudi Arabia kuwapa silaha wapiganaji wa Kikurdi wanaopambana vita vya Syria.