SYRIA-SIASA-USALAMA

Erdogan akutana na wenzake kutoka Urusi na Iran kuhusu Syria

Erdogan awapokea wenzake wa Urusi Putin na Rohani wa Iran kuhusu hatima ya Syria.
Erdogan awapokea wenzake wa Urusi Putin na Rohani wa Iran kuhusu hatima ya Syria. AFP

Viongozi wa Urusi, Iran na Uturuki wamekutana leo Jumatano katika mji wa Ankara kujadili kuhusu ufumbuzi wa mgogoro wa Syria, ambapo nchi hizi tatu zimejitokeza kama vigogo katika mgogoro huo.

Matangazo ya kibiashara

Marais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, wa Urusi Vladimir Putin na wa Iran Hassan Rouhani wameongea kwa dakika chache mbele ya vyombo vya habari kabla ya kuanza mazungumzo katika ikulu ya rais mjini Ankara.

Moscow na Tehran, ambazo zinasaidia serikali ya Damascus na Ankara, ambayo inasaidia waasi wa Syria, ni wadhamini wa mchakato wa Astana ambao umewezesha kutengwa kwa "maeneo manne" ambapo hapatakiwi kuepo na mapigano kwa lengo la kupunguza mapigano nchini Syria.

Lakini jitihada kwa utatuzi wa mgogoro wa Syria, uliosababisha zaidi ya watu 350,000 kupoteza maisha tangu mwaka 2011, zinaendelea kukwama kutokana na maslahi tofauti ya kila upande kutoka Moscow, Ankara na Tehran na tofauti juu ya hatima ya rais wa Syria Bashar al-Assad.

Mkutano wa mwisho kati ya viongozi hawa watatu kuhusu Syria ulifanyika Novemba 22 katika mji wa Sochi, mkutano ambao haukuzaa matunda yoyote.

Madhumuni ya mkutano huu wa pande tatu ni "kujipanga vizuri na kuanza mazungumzo ya maeneo ya ushawishi" na "kufikiria mustakabali wa eneo la kaskazini mwa Syria, baada ya kuondoka kwa askari wa Marekani," chanzo kilio karibu ya mazungumzo hayo kimesema.