SYRIA-ISRAEL-USALAMA

Syria na Urusi zashtumu Israel kuendesha shambulizi dhidi ya uwanja wa ndege wa kijeshi wa T-4

Ndege ya kivita F-15 ya Israel ikipaa hewani.
Ndege ya kivita F-15 ya Israel ikipaa hewani. AFP/JACK GUEZ

Urusi na Syria zimeishtumu Israelikuendesha mashambulizi dhidi ya uwanja wa ndege wa kijeshi usiku wa Jumapili kuamkia leo Jumatatu katikati mwa Syria.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, ndege mbili za kivita za Israel zilirusha makombora katika uwanja huo usiku wa leo Jumatatu. Makombora matano miongoni mwa makombora hayo yaliharibiwa,Urusi imesema. Israel imeendelea kusalia kimya.

Urusi na Syria zimeishtumu Israelikuendesha mashambulizi dhidi ya uwanja wa ndege wa kijeshi usiku wa Jumapili kuamkia leo Jumatatu katikati mwa Syria.Lakini baada ya Ufaransa na Marekani kukanusha madai hayo, lawama zimeanza kutolewa dhidi ya nchi hizi.

Tangu asubuhi hii, jeshi la Israeli halijaeleza chochote kufuatia shutma za Urusi na Syria dhidi yake.. "Tunachunguza suala hili" msemaji wa jeshi la Israel ameimbia RFI. Lakini kambi hii ya T-4 tayari ililengwa na mashambulizi mawili ya Israel.

Shambulizi la mwisho lililotokea mnamo mwezi wa Februari 2018, lilikua la kulipiza kisasi kwakuingia kwa ndege isiyokua na rubani ya Iran katika anga za Israel. Shambulizi la kwanza lilitokea mnamo mwezi Machi 2017.