URUSI-UJERUMANI-SYRIA-USHIRIKIANO

Putin azungumza kwa simu na Merkel kuhusu Syria

Rais wa Urusi Vladimir Putin amezungumza Jumanne wiki hii na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuhusu swala la Syria na swala la bomba la gesi la Nord Stream 2, ikulu ya Kremlin imetangaza.

Rais wa Urusi amemwambia Kansela wa Ujerumani, katika mazungumzo yao ya simu, kwamba mashambulizi yaliyoendeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Syria yalikiuka sheria ya kimataifa na yamevuruga mchakato wa amani.
Rais wa Urusi amemwambia Kansela wa Ujerumani, katika mazungumzo yao ya simu, kwamba mashambulizi yaliyoendeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Syria yalikiuka sheria ya kimataifa na yamevuruga mchakato wa amani. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi, amesema, alimwambia Kansela wa Ujerumani kuwa mashambulizi ya anga yaliyofanywa mwishoni mwa wiki hii iliyopita na Marekani, Ufaransa na Uingereza nchini Syria ni kinyume na sheria ya kimataifa na yamevuruga mchakato wa amani.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Berlin wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa New Zealand, Angela Merkel ameshtumu Urusi kuhusika kwa njia moja ama nyingine katika mashambulizi ya kemikali yalitekelezwa Aprili 7 katika mji wa Duma, mashariki mwa Damascus, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea na mazungumzo na Moscow.

"Tunajua kwamba kuhusu mashambulizi ya gesi yenye sumu nchini Syria, Urusi, kama mshirika wa Assad, inahusika kwa njia fulani, hakuna shaka juu ya swala hili, lakini ni muhimu kuendelea kuzungumza na Urusi, " Angela Merkel amesema.

Heiko Maas, Waziri wa mambo ya Kigeni wa Ujerumani, pia amesisitiza juu ya kuendeleza mazungumzo na kuhusu nafasi ya mpatanishi ambapo Berlin inaweza kuchukua nafasi hiyo katika mgogoro wa Syria.

Kuzindua mchakato wa amani itakuwa mojawapo ya mada muhimu ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka kundi la nchi zilizostawi kiuchumi (G7) mwishoni mwa wiki hii huko Toronto. "Tunapaswa kutumia fursa hii kufufua mchakato wa kisiasa (...) Tunahitaji pia Urusi kwa mazungumzo haya," amesema waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, ambaye alizungumza pamoja na mwenzake wa Canada Chrystia Freeland.