ISRAEL-AFRIKA-WAHAMIAJI-USALAMA

Israel yafuta hatua yake ya kuwafukuzi wahamiaji kutoka Afrika

Wakimbizi wa Afrika hasa kutoka Eritrea na Sudan huko Tel Aviv, Israeli.
Wakimbizi wa Afrika hasa kutoka Eritrea na Sudan huko Tel Aviv, Israeli. AFP/Yehuda RAIZNER

Israel imesema haitawafukuza tena wahamiaji haramu kutoka barani Afrika walioingia nchini humo kinyume cha sheria, baada ya hatu hiyo kukosolewa kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilikuwa imepanga kuwafukuza wahamiaji 42,000 kutoka Eritrea na Sudan, lakini imesachana na mpango huo baada ya kukosa nchi ya kuwapeleka.

Awali ilitangaza kwamba ilisaini makubaliano na Umoja wa Mataifa kuwahamisha baadhi ya wahamiaji hao katika nchi za Magharibi.

"Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya wakimbizi na Israel wamefikia makubaliano kuruhusu kuondoka kwa wahamiaji takriban16,250 wa Afrika kwenda nchi za Magharibi, huku serikali ya Israeli ikitakiwa kuwapa hifadhi ya ukimbizi wahamiaji wengine watakaosalia nchini humo" , taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilisema.

Hivi karibuni mamia ya wahamiaji wa Afrika waliamua kufanya mgomo wa kususia chakula wakati ambapo serikali ya Israel ilikua ikiendesha operesheni ya kuwakamata wahamiaji kulingana na mpango wake tata na kuwataka kuchagua kuondoka nchini humo au kufungwa jela

Umoja wa Mataifa ulikua uliitaka Israel kuachana na mpango huo wa kuwafukuza maelfu ya wahamiaji kutoka Afrika.

Mpango huo ulikua unahusisha wahamiaji 38,000, hasa kutoka Eritrea na Sudan.

Kabla ya hatua hii, Rwanda na Uganda zilikuwa zimetajwa kuwa tayari kuwakubali wahamiaji hao, taarifa ambazo hata hivyo zimekuwa zikikanushwa na nchi hizo mbili.

Nchi nyingi na mashirika ya haki za binadamu yamekua yakikoso hatua ya Israel ya kuwafukuza kwa nguvu wahamiaji wa kiafrika nchini humo.