PALESTINA-PLO-SIASA-USALAMA

Abbas achaguliwa tena kama mwenyekiti wa kamati tendaji ya PLO

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.
Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas. REUTERS/Mohamad Torokman

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, amechaguliwa tena kama mwenyekiti wa kamati tendaji ya chama cha PLO. Uchaguzi huo umefanyika Ijumaa wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 anajaribu kuanzisha upya majukumu yake, huku akiwateua washirika wake wa karibu katika nafasi muhimu.

Uchaguzi huu, uliosubiriwa kwa hamu na gamu, unakuja baada ya mkutano wa siku nne wa Baraza la kitaifa la Palestina (PNC) uliyofanyika Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi.

Mkutano wa PNC, ambao ni wa kwanza katika miaka 22, uliitishwa na Mahmoud Abbas ili kuanzishwa kwa mkakati wa kukabiliana na uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kuitambua Jerusalemu kama mji mkuu wa Israeli na kuhamisha ubalozi wa Marekani katika mji huo.

Mahmoud Abbas ameshtumiwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kama mtu mwenye ubaguzi mwenye kuchochea uhasama baada ya kiongozi wa Palestina kusema Jumatatu wiki hii wakati wa hotuba yake ya kufungua mkutano wa PNC kwamba Wayahudi waliiteswa huko Ulaya sio kwa sababu ya dini yao lakini kwa sababu ya shughuli zao katika kuvaa na benki.