MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Marekani kufungua ubalozi mpya Jerusalem

Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na Naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni John Sullivan pia watakuwa kwenye sherehe hya ufunguzi wa ubalozi mpya wa Marekani, Jerusalem..
Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na Naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni John Sullivan pia watakuwa kwenye sherehe hya ufunguzi wa ubalozi mpya wa Marekani, Jerusalem.. REUTERS/Amir Cohen

Marekani inatarajia kufungua rasmi Jumatatu wiki hii ubalozi wake mpya Jerusalem, licha ya hatua hiyo kupingwa na jumuiya ya kimataifa na Palestina, hali ambayo huenda ikasababisha kuzuka kwa mvutano mkubwa wa kikanda.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa kadhaa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo. Binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner pia watahudhuria sherehe hiyo.

Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na Naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni John Sullivan pia watakuwa kwenye sherehe hiyo.

Ufunguzii huu utaendana na kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 70, kulingana na kalenda ya Gregory, ya kuundwa kwa taifa la Israeli. Jumanne wiki hii, Wapalestina wataadhimisha "Nakba" ("Mateso" katika ulimwengu wa Kiarabu), kuondoka kwa mamia ya maelfu yao baada ya kufukuzwa au kuyahama makazi yao mnamo mwaka 1948.

Ufunguzi huo utafanyika katika wakati ambapo mvutano kati ya Israeli na Palestina unaendelea. Wapalestina wamekuwa wakiandamana kwa wiki kadhaa katika Ukanda wa Gaza wakitaka iheshimiwe mipaka ya mwaka 1948.

Hatua ya Marekani ya kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem ni katika kutekeleza ahadi ya Rais Donald Trump Desemba 6 ya kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli.

Rais Trump anatarajiwa kuhutubia wale ambao watahudhuria sherehe hiyo kwa njia ya video.

Hatua ya Marekani ya kufungua ubalozi wake Jerusalem imekaibishwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa.

Wapalestina wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye.

Israel ilichukua udhibiti wa eneo la Jurusalem mashariki mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya kati, na inahutaja mji huo kuwa wake na usiogawanwa.

Wapalestina zaidi ya 50 wameuawa na jeshi la Israeli wakati wa maandamano yaliyoanza tangu Machi 30.