AFGHANISTAN-USALAMA

Waziri wa mambo ya ndani wa Afghanistan alengwa katika shambulizi

Des policiers afghans montent la garde à Kaboul, après une attaque contre le ministère de l'Intérieur, le 30 mai 2018.
Des policiers afghans montent la garde à Kaboul, après une attaque contre le ministère de l'Intérieur, le 30 mai 2018. REUTERS/Mohammad Ismail

Waziri wa mambo ya ndani wa Afghanistan ameponea kuuawa baada ya kundi la watu wenye silaha kupenya na kuingia katika jengo la wizara hiyo. Lakini hali imeanza kuwa shwari.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa idara ya usalama mjini Kabul, kundi la watu wanne wenye silaha ndio waliongoza shambulio hilo, ambapo milio ya risasi na milipuko vilisikika karibu na jengo hilo la wizara ya mambo ya ndani.

Milipuko kadhaa ililenga kituo cha polisi kwenye jengo la wizara ya mambo ya ndani, linalopatikana kwenye barabara inayoelekea kwenye uwanja wa ndege wa Kabul saa 12:30 (saa za Afghanistan).

Washambuliaji wanne walifaulu kuingia katika jengo la wizara ya mambo ya ndani. Vikosi vya usalama vilitumwa kukabiliana na hali hiyo. wakati huo kulikua na ubadilishanaji risasi kati ya kundi hilo la washambuliaji na vikosi vya usalama vya serikali. Eneo la tukio lilikua bado likizingirwa na vikosi vya usalama mapema mchana.

Hata hivyo, hakuna taarifa za vifo, lakini kwa muijbu wa chanzo cha polisi, polisi mmoja amejeruhiwa. Mkuu wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba washambuliaji wote wameuawa.