YEMEN-UAE-USALAMA

UAE yawataka waasi wa Houthi kuondoka bila masharti Hodeida

Majeshi ya Yemeni kusini mwa uwanja wa ndege wa Hodeida.
Majeshi ya Yemeni kusini mwa uwanja wa ndege wa Hodeida. AFP

Umoja wa Falme za Kirabu, UAE, nguzo ya muungano wa nchi zinazopambana dhidi ya waasi nchini Yemen umewataka waasi wa Houthi kuondoka bila masharti katika mji wa Hodeida, kwa ajili ya kuingizwa kwa misaada ya kibinadamu.

Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, Martin Griffith, alikutana kwa mazungumzo Jumapili katika mji wa Sanaa na viongozi wa waasi, kama sehemu ya upatanishi unaolenga kusitisha mapigano na kuzuia janga jipya la kibinadamu katika nchi hiyo. Anatarajiwa Jumatatu wiki hii kutoa taarifa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Katika uwanja wa vita, kusini mwa uwanja wa ndege wa Hodeida, askari saba wa serikali na waasi 18 waliuawa katika ubadilishanaji risasi,vyanzo vya kijeshio vimebaini leo Jumatatu. Mpaka sasa waasi na askari 164 wameuawa katika vita hivyo vinavyoendelea.

"Operesheni ya kijeshi ya (kudhibiti) bandari ya Hodeida itaendelea mpaka waasi waondoka bila masharti," Waziri wa Mambo ya Nje wa Falme za Kiarabu Anwar Gargash amesema mbele ya vyombo vya habari.