Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-MAZUNGUMZO-USALAMA

Mazungumzo kati ya Urusi na waasi wa Syria yavunjika

Wakaazi wa mkoa wa Deraa wakiendelea kuyatoroka makaazi yao, Juni 29, 2018.
Wakaazi wa mkoa wa Deraa wakiendelea kuyatoroka makaazi yao, Juni 29, 2018. REUTERS/Alaa Al-Faqir

Mazungumzo kati ya wapiganaji wa upinzani nchini Syria na Urusi, kusitisha mapigano Kusini mwa nchi hiyo yamevunjika. Hii si mara ya kwanza mazungumzo kati ya pande hizo mbili kuvunjika, kubaada ya lawama kutoka kila upande.

Matangazo ya kibiashara

Upinzani umeishtumu Urusi kwa kusababisha mazungumzo hayo kuvunjika baada ya kukataa pendekezo la kuondoka kwa wanajeshi wa Syria na wapiganaji wa Iran katika ngome zake.

Mapigano yameendelea kushuhudiwa nchini katika ngome za upinzani kama Deraa, Tafas na Saida na kusababisha vifo vya mamia ya raia katika siku za hivi karibuni.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu alisema nchi yake imekubaliana na Urusi na vilevile Iran kuwe na ushirikiano wa karibu katika lengo la kutafuta amani ya kudumu huko Syria.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.