SYRIA-USALAMA

Maelfu ya watu wanahitaji kuhamishwa kutoka Fuaa na Kafraya

Mji waasi wa Madaya, kusini magharibi mwa Syria, umezingirwa kwa miezi sita na jeshi la Bashar Al Assad.
Mji waasi wa Madaya, kusini magharibi mwa Syria, umezingirwa kwa miezi sita na jeshi la Bashar Al Assad. REUTERS/Omar Sanadiki

Mwafaka umefikiwa nchini Syria, kuwaruhusu maelfu ya raia kuondoka katika miji ya Fuaa na Kafraya, yanayoendelea kushuhudia mapigano kati ya wanajeshi na wapiganaji wa upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Waangalizi wa mzozo wa Syria, wameeleza kuwa, makubaliano hayo yanawataka wakaazi wa miji hiyo miwili, kuondoka kabisa kabla ya vita kurejelewa tena katika mkoa huo wa Allepo.

Raia hao wanaondoka makwao wakiacha makaazi yao na kwenda kambini na maeneo mengine bila ya kuwa na mahitaji muhimu ya binadamu.

Mnamo mwaka 2016 Umoja wa Mataifa uliitaka serikali ya Syria kuwaruhusu takriban raia 400 kuondolewa kwa ndege kutoka mji wa Madaya ambako shirika la kimataifa la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF lilisema watu 28 walikufa njaa.

Urusi, Marekani na nchi za Mashariki ya kati yanahimiza kuwepo mazungumzo kati ya serikali ya Syria na upinzani lakini kuendelea kuwepo madarakani kwa Assad kunaonekana kuwa suala tete.