YEMEN-UN-USALAMA

Watoto 29 waangamia katika mashambulizi ya anga Yemen

Watoto waliojeruhiwa katika shambulio la nga la ndege za muungano wa nchi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Kihouthi, Alhamisi, Agosti 9, 2018.
Watoto waliojeruhiwa katika shambulio la nga la ndege za muungano wa nchi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Kihouthi, Alhamisi, Agosti 9, 2018. REUTERS/Naif Rahma

Umoja wa Mataifa untaka uchunguzi binafsi na wa haraka kufanyika baada ya kutokea kwa shambulizi la bomu Kaskazini mwa Yemen na kuwauwa watoto 29.

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress ametoa wito huo, huku akitoa wito kwa pande zote zinazohusika katika vita nchini humo kuheshimu sheria za Kimataifa.

Aidha, Guteress asema ni muhimu sana kwa wanaopigana kuhakikisha kuwa hawawalengi raia wa kawaida na kutozuia misaada ya kibinadamu kuwafikia.

Wito huu umekuja wakati huu muungano wa nchi zinazoongozwa na Saudi Arabia kushukiwa kuwa nyuma ya shambilizi hilo baya katika siku za hivi karibuni.

Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema wanajeshi hao wakiongozwa na Saudi Arabia walilenga basi lilolokuwa na wanafunzi katika eneo hilo ambalo lina waasi wa Kihouthi.

Shirika la Kimataifa la msalaba mwekundi limesema watoto wote waliopoteza maisha, walikuwa chini ya miaka 15.