SYRIA-UFARANSA-UJERUMANI-UTURUKI-URUSI-USALAMA

Urusi, Ufaransa, Uturuki na Ujerumani waandaa mkutano kuhusu Syria

Waziri wa mambo ya Nje wa Urusi Sergueï Lavrov anatarajiwa kuwa Ujerumani kwa mazungumzo na mwenzake kuhusu Syria..
Waziri wa mambo ya Nje wa Urusi Sergueï Lavrov anatarajiwa kuwa Ujerumani kwa mazungumzo na mwenzake kuhusu Syria.. REUTERS/Sergei Karpukhin

Mkutano unaojumuisha nchi nne kuhusu Syria ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Uturuki na Ujerumani "unatarajiwa hivi karibuni," Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov anatarajiwa Jumatatu wiki hii huko Ankara kwa ziara ya siku mbili kuandaa mkutano huo, serikali ya Moscow imesema.

Suala kuhusu Syria lilikuwa kwenye agenda ya mazungumzo ya simu kati ya Vladimir Putin na Emmanuel Macronsiku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Mazungumzo yanaendelea kuhusu kiwango na muundo wa mkutano huo, chanzo kutoka ikulu ya Elysee kimebaini. "Mkutano huo utahusu tu nasaha," chanzo hicho kimesema.

Duru kutoka Berlin zinasema kuwa ofisi ya kansela wa Ujerumani imetangaza kwamba rais wa Urusi atapokelewa siku ya Jumamosi na Angela Merkel katika ikulu ya Meseberg, karibu na mji mkuu wa Ujerumani.

Wawili hawa watajadili hasa suala kuhusu Syria, lakini pia masuala yanayohusiana na Ukraine na nishati, amesema msemaji wa serikali ya Ujerumani.