AFGHANISTAN-MAREKANI-NATO-USALAMA

Mkuu wa Pentagon James Mattis azuru Afghanistan

Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis. REUTERS/Aaron P. Bernstein

Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis na Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo Joseph Dunford wamewasili Kabul Ijumaa wiki hii kukutana na kamanda mpya wa majeshi ya NATO nchini Afghanistan, Jenerali Scott Miller.

Matangazo ya kibiashara

Swala la mazungumzo ya amani na Taliban pia litajadiliwa, kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi cha Marekani.

Juma lililopita Urusi ilikubali, kwa ombi la Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani, kuahirisha tarehe ya mkutano wa amani kuhusu Afghanistan uliokua ulipangwa kufanyika Septemba 4 huko Moscow, ambapo wapiganaji wa Taliban walikubali kwenda.

Mwezi Agosti mwaka jana Rais wa Marekani Donald Trump alisema kuwa mpango wake ulikuwa ni wa kuondoa vikosi vya Marekani, lakini badala yake ameamua wanajeshi hao kubakia ili kuzuia kurudia makosa ambayo yalitokea nchini Iraq.

Alisema pia kuwa anaongeza idadi ya wanajeshi watakao pelekwa nchini Afghanstan.

“Kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini Afghanistan kutawapa nafasi magaidi kujidhatiti vilivyo, ” alisema wakati huo Bw Trump.

Bw Trump alisisitiza kuwa kitendo cha Marekani kujiondoa kwa haraka nchini Afghanistan, kitatatoa nafasi kwa ugaidi kujiimarisha zaidi kama ilivyotokea nchini Iraq.