AFGHANISTAN-IS-TALIBAN-USALAMA

Watu zaidi ya 20 waua katika shambulizi la kujitoa mhanga Afghanistan

Mashambulizi ya kujitoa mhanga yanaendelea kuathiri mji mkuu wa Jalalabad, Afghanistan.
Mashambulizi ya kujitoa mhanga yanaendelea kuathiri mji mkuu wa Jalalabad, Afghanistan. REUTERS/Parwiz

Mfululizo wa mashambulizi yaliyokumba eneo la Mashariki mwa Afghanistan Jumanne wiki hii yameua watu zaidi ya 20 miongoni mwa waandamanaji karibu na mpaka wa Pakistani na mbele ya shule ya wasichana.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo baya ilitokea saa saba saa za Afghanistan (sawa na saa 08:30 asubuhi saa za kimataifa), kwenye mpaka kati ya Afghanistan na Pakistan wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga alilipua mkanda wake katikati ya umati wa waandamanaji, karibu kilomita 70 kutoka mji wa Jalalabad.

Waandamanaji walizuia barabara kati ya nchi hizo mbili wakipinga uteuzi wa mkuu mpya wa polisi. Watu wasiopungua 19 wameuawa na 51 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa msemaji wa Gavana wa mkoa wa Nangarhar Ataullah Khogyani.

Saa chache kabla, mashambulizi mawili yalilenga shule ya wasichana katika mji mkuu wa Jalalabad, na kuua mtu mmoja na kuwajeruhi wanne.

Bomu la kwanza lililipuka mbele ya shule ya wasichana ya Malika Omaira karibu saa 08:30 asubuhi. Mlipuko wa pili ulitokea baada ya wanafunzi wa shule jirani ya wavulana walikua wakikimbilia kwenye eneo la kwanza la tukio.

Hakuna kundi ambalo limedai kuhusiika na mashambulizi, wakati kundi la Islamic State (IS) na Taliban wanaendesha harakati zao katika eneo hilo nchini Afghanistan.

Makundi haya mawili yanapinga elimu kwa wanawake. Walilazimisha kufungwa kwa shule nyingi za wasichana nchini Afghanistan.