AFGHANISTAN-IS-TALIBAN-USALAMA

Idadi ya vifo katika mashambulizi yafikia 68 Afghanistan

Idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi ya kujitoa mhanga, yaliyotokea Jumanne wiki hii katika mkoa wa Nangarhar, mashariki mwa Afghanistan imefikia 68 kwa mujibu wa viongozi wa mkoa huo.

Watu wengi waangamia katika mashambulizi ya kujitoa mhanga, Nangarhar, mashariki mwa Afghanistan.
Watu wengi waangamia katika mashambulizi ya kujitoa mhanga, Nangarhar, mashariki mwa Afghanistan. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Watu 165 walijeruhiwa katika mashambuloizi hayo ambayo yamewaacha watoto wengi mayatima.

Awali serikali ilitangaza kwamba watu 32 ndio waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua miongoni mwa umati wa watu waliokusanyika kwa maandamano dhidi ya kamanda wa wanamgambo wenye silaha katika mkoa huo.

Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na mashambulizi haya. Kundi la Taliban limetoa taarifa likikanusha kuhusika na mashambulizi hayo.

Mkoa wa Nangarhar, kwenye mpaka na Pakistan, tangu mwanzoni mwa mwaka 2015 ni mojawapo ya ngome za kundi la Islamic State nchini Afghanistan.