IRAQ-USALAMA

Sita wauawa katika shambulio la kujitoa mhanga Tikrit

vikosi vya usalama na ulinzi vimeendelea kuigana na wapiganaji kutoa makundi ya waasi.
vikosi vya usalama na ulinzi vimeendelea kuigana na wapiganaji kutoa makundi ya waasi. REUTERS/Mushtaq Muhammed

Shambulizi la kujitoa mhanga limeua watu sita na wengine kujeruhiwa Jumatato wiki hii katika mgahawa mmoja karibu na Tikrit, nchini Iraq, polisi imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Mgahawa ambao umeshambuliwa umekua ukitembelewa na maafisa wa vikosi vya usalama na wanamgambo wanaosaidia jeshi katika vita dhidi ya makundi ya wassi, hasa makundi ya wanajihadi, polisi imesema.

Wengi wa waathirika ni watalii wa Iraq ambao walikuwa katika basi iliyosimama karibu na mgahawa, imesema polisi na chanzo cha hospitali.

Hakuna kundi ambalo limedai kutekeleza shambulizi hilo.