SYRIA-URUSI-UTURUKI-IRAN-USALAMA

Iran yakaribisha mkataba kati ya Urusi na Uturuki kuhusu Idlib

Iran imekaribisha mkataba kati ya Uturuki na Urusi kuhusumkoa wa Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria, kituo cha Lebanoni cha Al Maïadine kimeripoti Jumanne wiki hii.

Rais aw Urusi Vladimir Putin (kushoto) na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kutia saini mkataba kati ya nchi hizo mbili, tarehe 6 Agosti.
Rais aw Urusi Vladimir Putin (kushoto) na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kutia saini mkataba kati ya nchi hizo mbili, tarehe 6 Agosti. (Photo : Umit Bektas/Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Kituo hicho kikimnikuu msemaji wa wizaraya mambo ya nje ya Iran, kimesema Iran inaungana na Urusi na Uturuki kwa mkataba huo.

Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan walifikia mkataba siku ya Jumatatu kuhusu kuundwa kwa eneo lenye ambalo halitakiwi kuwepo na askari kutoka nchi yoyote ili kutenganisha vikosi vya serikali na waasi.

Eneo hili litaundwa katikati ya mwezi wa Oktoba na waasi wa "msimamo mkali", ikiwa ni pamoja na Al-Nusra Front, hawatahusishwa na watatakiwa kuondoka mara moja katika mkoa huo.