URUSI-SYRIA-JESHI

Putin asema kuangushwa kwa ndege ya kijeshi ilikuwa ni bahati mbaya

Ndege ya kivita ya Urusi
Ndege ya kivita ya Urusi 路透社。

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuangushwa kwa ndege ya kijeshi ya nchi yake na wanajeshi wa Syria, lilikuwa ni tukio lililotokea kwa bahati mbaya.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imekuja, baada ya Wizara yake ya ulinzi kuishtumu Israel kwa kuiangusha ndege hiyo na kusababisha wanajeshi wote 15 wa Urusi kuangamia.

Matamshi ya rais Putin yamelenga kutoharibu uhusiano kati ya nchi yake na Israel.

Israel imekuwa ikitishia kuwa itaangusha ndege yoyote ya kivita, itakayoonekana katika anga lake kwa sababu za kiusalama.

Syria imekuwa ikisema Israel ni adui wake na ndio sababu ililenga ndege hiyo, ikifikiria ni ya Israel.

Limekuwa tukio la kwanza kwa Syria kuiangusha ndege ya Urusi.

Urusi ilituma wanajeshi wake nchini Syria mwaka 2015, kusaidia serikali ya rais Bashar Al Assad kupambana na makundi ya kigaidi.