SAUDI ARABIA-MAREKANI-UTURUKI-UCHUNGUZI

Saudi Arabia yaingia matatani baada ya kutoweka kwa Jamal Khashoggi

Mwandishi wa habari Jamal Khashoggi alitoweka Jumatano wiki iliyopita baada ya kwenda wenye balozi wa Saudi kutafuta vibali vya ndoa kati yake na mchumba wake raia wa Uturuki , Hatice Cengiz.
Mwandishi wa habari Jamal Khashoggi alitoweka Jumatano wiki iliyopita baada ya kwenda wenye balozi wa Saudi kutafuta vibali vya ndoa kati yake na mchumba wake raia wa Uturuki , Hatice Cengiz. Middle East Monitor/Handout via REUTERS

Marekani imetaka uchunguzi wa kina ufanyike ili kuhakikisha wapi aliko mwandishi wa habari, raia wa Saudi Arabia, aliyetoweka tangu Jumatano wiki iliyopita nchini Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani alisema "ana wasiwasi" kuhusu hatima ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari aliyekuwa akitumikia gazeti la Washington Post.

Mwanadishi huyo wa habari alitoweka Jumatano wiki mbilizi zilizopita baada ya kwenda katika ubalozi wa Saudi Arabia huko Istanbul, nchini uturuki, ambako alikuwa alikuja kutafuta vibali vya ndoa kati yake na mchumba wake raia wa Uturuki, Hatice Cengiz, kufuatia kuvunjika kwa ndoa yake ya awali. Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari kutoka Saudi Arabia, mkosoaji mkubwa wa utawala wa kifalme nchini hmu, aliitoroka nchini yake mwaka jana na kukimbilia nchini Marekani kwa hofu ya kukamatwa.

"Nina wasiwasi kuhusu kutoweka kwa mwandisi huyo wa habari. Siipendi kusikia kuhusu matukio kama hayo. Kwa sasa hakuna mtu anayejua kilichotokea. Taarifa mbaya zimekuwa zikisambazwa. Siipendi mambo hayo, "amesema Donald Trump akihojiwa kuhusu hatima ya mwandishi wa habari aliyetoweka.

Mwandishi huyo, raia wa Saudia, Jamal Khashoggi kwa mara ya mwisho alionekana katika jengo la ubalozi wa Saudi Arabia wiki iliyopita.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameitaka Saudia kutoa ushahidi kuhusiana na mwandishi wa habari aliyepotea kwamba alitoka nje ya majengo ya ubalozi wao mjini Istanbul.

Uturuki imeomba kufanya uchunguzi ndani ya majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia, kwa madai kuwa Khashoggi aliuawa ndani ya majengo hayo kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.