SAUDI ARABIA-MAREKANI-UTURUKI-UCHUNGUZI

Trump: Saudi Arabia ichukuliwe kama haina hatia

Polisi wa Uturuki wanasubiri kuwasili kwa polisi wa masuala wa kisayansi mbele ya makazi ya balozi mdogoi wa Saudi Arabia  Istanbul Oktoba 16, 2018.
Polisi wa Uturuki wanasubiri kuwasili kwa polisi wa masuala wa kisayansi mbele ya makazi ya balozi mdogoi wa Saudi Arabia Istanbul Oktoba 16, 2018. REUTERS/Murad Sezer

Rais wa Marekani sasa anasema Saudi Arabia isionekane kama ilihusika na kutoweka na uwezekano wa kuuawa kwa Mwanahabari Jamal Khashoggi, alipotembelea ubalozi wa nchi yake jini Instanbul nchini Uturuki, wiki mbli zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Trump ameliambia Shirika la Habari la Associated Press kuwa, uongozi wa Saudi Arabia umeonekana kuhusika, kabla ya hilo kuthibitishwa.

Kiongozi huyo ameonekana kubadilisha kauli hiyo, baada ya ziara ya Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Mike Pompeo jijini Riyadh, ambaye baada ya kukutana na Mfalme Salman, amesema Saudi Arabia ina nia ya dhati kutaka kufahamu aliko Mwanahabari huyo ambaye ni raia wake.

Hata hivyo Maseneta wa Marekani wameomba Saudi Arabia ichukuliwe vikwazo.

Wiki iliyopita Marekani ilitaka uchunguzi wa kina ufanyike ili kuhakikisha wapi aliko mwandishi wa habari, raia wa Saudi Arabia, aliyetoweka tangu Jumatano wiki mbili zilizopita nchini Uturuki.

Rais wa Marekani alisema "ana wasiwasi" kuhusu hatima ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari aliyekuwa akitumikia gazeti la Washington Post.

Hivi karibuni Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliitaka Saudia kutoa ushahidi kuhusiana na mwandishi wa habari aliyepotea kwamba alitoka nje ya majengo ya ubalozi wao mjini Istanbul.

Mwanadishi huyo wa habari alitoweka Jumatano wiki mbilizi zilizopita baada ya kwenda katika ubalozi wa Saudi Arabia huko Istanbul, nchini uturuki, ambako alikuwa alikuja kutafuta vibali vya ndoa kati yake na mchumba wake raia wa Uturuki, Hatice Cengiz, kufuatia kuvunjika kwa ndoa yake ya awali. Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari kutoka Saudi Arabia, mkosoaji mkubwa wa utawala wa kifalme nchini hmu, aliitoroka nchini yake mwaka jana na kukimbilia nchini Marekani kwa hofu ya kukamatwa.