Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-MAREKANI-UTURUKI-UCHUNGUZI

Washington Post yachapisha makala ya mwisho aliyoandika Jamal Khashoggi

Makao makuu ya Gazeti la Washington Post.
Makao makuu ya Gazeti la Washington Post. AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Gazeti la Washington Post limechapisha makala ya mwisho yaliyoandikwa na bwana Khashoggi kabla ya kutoweka kwake. Katika makala hayo Jamal Khashoggi anazungumzia umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika eneo la Mashariki ya kati.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump, amekanusha madai kuwa anajaribu kuutetea uongozi wa Saudi Arabia kuhusu madai ya kuuawa kwa Mwanahabari Jamal Khashoggi.

Trump amesema anachosubiri ni ukweli kuhusu kilichompata Khashoggi, ambaye Uturuki inasema ina ushahidi kuwa aliuawa akiwa ndani ya Ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Instabul na sasa Marekani inataka mkanda kuonesha namna mwanahabari huyo alivyouzwa.

Wiki iliyopita Donald Trump aliwaomba watu kutokimbia kuwalaumu viongozi wa Saudia kabla ya kuthibitisha kuhusika kwa viongozi hao katika kisa hiki

Saudi Arabia imekanusha kuhusika na mauaji ya Khashoggi ambaye tangu kuotoweka kwake, alikuwa anaandika makala ya kuukosoa uongozi wa nchi yale.

Hata hivyo Marekani imeomba Uturuki kutoa ushahidi wa kanda ya sauti inayodai kuwa Jamal Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.