MAREKANI-SAUDI ARABIA-MWANAHABARI

Mwanamfalme wa Saudi Arabia asema waliomuua Khashoggi watachukuliwa hatua

Mwanamfalme wa Saudi Arabia ameapa nchi yake kuchukua hatua kali dhidi ya watuhumiwa waliohusika katika mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi, ambaye aliuawa kwenye ubalozi wa nchi hiyo mjini Istanbul, Uturuki.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman BANDAR AL-JALOUD / Saudi Royal Palace
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa kongamano la kiuwekezaji mjini Riyadh, mwanamfalme Mohammed bin Salman, amesema kitendo kilichofanywa hakivumiliki na kwamba nchi yake haitaruhusu kutokea mgogoro kati yake na Uturuki.

Utawala wa Riyadhi umeendelea kukanusha kuwa mwanamfalme Salman alikuwa na mkono katika kuagiza mauaji ya Khashoggi.

Siku ya Jumanne ya wiki hii, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema mwanahabari Khashoggi ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Riyadhi, alikuwa muhanga wa mauaji yaliyopangwa kisiasa na majasusi wa Saudi Arabia.

Haya yanajiri wakati huu mataifa kadhaa ya Ulaya yakiwa tayari kutangaza vikwazo dhidi ya wahusika.