Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Sita waangamia katika shambulizi la kujitoa muhanga Afghanistan

Askari wa Afghanistan mjini Kabul.
Askari wa Afghanistan mjini Kabul. REUTERS/Omar Sobhani
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Watu wasiopungua sita wameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa leo Jumatano katika shambulizi la kujitoa muhanga lililotokea mbele ya lango la jela kubwa zaidi nchini Afghanistan, mashariki mwa mji mkuu Kabul, maafisa wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Hakuna kundi hata moja ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghamistan, mshambuliaji wa kujitoa muhanga alijilipua karibu ya gari la mfanyakazi wa jela hilo.

Watu sita wamefariki dunia karibu na lango la jela na wengine watatu wamejeruhiwa, afisa mwingine wa serikali amesema.

Jela la Pul-i-Charki linawafungwa zaidi ya mia moja, ikiwa ni pamoja na waasi wa Taliban.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.