UTURUKI-SAUDI ARABIA-JAMAL-HAKI

Uturuki yadai kuwa Khashoggi alinyongwa katika ubalozi mgodo a Saudia

Mmoja wa waandamanaji akishikilia picha ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi nje ya ubalozi mdogo wa Saudi Istanbul tarehe 25 Oktoba 2018.
Mmoja wa waandamanaji akishikilia picha ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi nje ya ubalozi mdogo wa Saudi Istanbul tarehe 25 Oktoba 2018. REUTERS/Osman Orsal

Uturuki inasema Mwanahabari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi alinyongwa, pindi tu alipoingia katika Ubalozi wa nchi yake mjini Istanbul katika mauaji ambayo Ankara inasema yalipangwa.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Mkuu wa Mashtaka ya umma imesema kuwa, baada ya Khashoggi kunyongwa, mwili wake ulikatwakatwa.

Saud Al-Mujab, Mkurugenzi Mkuu wa mashtaka nchini Saudi Arabia yupo nchini Uturuki, kuchunguza kilichotokea wakati huu Uturuki ikisema haioni iwapo Saudi Arabia ipo tayari kutoa ushirikiano.

Bw Khashoggi, mkosoaji wa Serikali ya Saudi Arabia, alitoweka tarehe mbili Oktoba baada ya kuingia ubalozi wa Saudia mjini Istanbul.

Saudi Arabia inasema kuwa madai kuwa iliamrisha kuuliwa kwa Bw Khashoggi si ya ukweli.

Uturuki inadai kuwa ina sauti na video zinazoonyesha kuwa mwandishi wa habari raia wa Saudi Arabia aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia nchini Istanbul mapema mwezi huu kwa mujibu wa maafisa wa Marekani na Uturuki walionukuliwa na gazeti la Washington Post.

Mwandishi huyo Jamal Khashoggi aliingia katika ubalozi huo ulio mjini Istanbul tarehe mbili Oktoba kwa minajili ya kupata stakabadhi ambazo zingemruhusu amuoe mchumba wake raia wa uturuki. Hajaonekana tangu wakati huo.

Sauti zilizorekodiwa zinatoa ushahidi kuwa kikosi cha watu kutoka nchini Saudi Arabia, kilichotumwa kwenda Istanbul kilihusika katika kumuua Khashoggi.

“Sauti iliyorekodiwa ndani ya ubalozi inafichua kile kilichomtendekea Jamal baada ya kuingia ubalozi huo wa Saudi Arabia.

“Unaweze kusikia sauti yake na sauti za wanaume wanaozungumza lugha ya kiarabu,” afisa mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina alinukuliwa akisema. “Unawezaa kusikia jinsi alihojiwa, kateswa na kuuliwa.”