AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Ishirini na mbili wauawa magharibi mwa Afghanistan

Askari wa Afghanistan wakitoa ulinzi katika mji wa Farah dhidi ya wapoganaji wa taliban Mei 2018.
Askari wa Afghanistan wakitoa ulinzi katika mji wa Farah dhidi ya wapoganaji wa taliban Mei 2018. HAMEED KHAN / AFP

Maafisa wa polisi zaidi ya Ishirini na mbili wameuawa katika shambulizi la Taliban katika jimbo linalokabiliwa na mdororo wa usalama la Farah, magharibi mwa Afghanistan.

Matangazo ya kibiashara

"Miili ishirini na miwili na polisi wawili waliojeruhiwa walisafirishwa katika Hospitali ya Farah. Wote waliuawa katika shambulizi, "amesema Dk Shir Ahmad Weda, ambaye ni kiongozi wa hospitali hiyo.

Kundi la Taliban lkimekiri kuhusika na shambulizi hilo, huku likibaini kwamba limeua maafisa wa polisi 25. "Magari manne yaliharibiwa vibaya na kiasi kikubwa cha silaha zimekamatwa," Qari Yousuf Ahmadi, msemaji wa wapiganaji wa Taliban amesema kupitia ujumbe wa WhatsApp.

Msemaji wa polisi Farah Mohibullah Mohib, kwa upande wake, amesem maafisa watano wa polisi wameuawa na 7 kumejeruhiwa katika shambulizi lililolenga msafara wa polisi katika wilaya ya Juwain. Vikosi cya usalama vya Afghanistan vimeendelea kutupilia mbali idadi iliyotolewa na kundi la Taliban kwamba maafisa wa polisi 25 wameuawa.

Polisi na jeshi mara kwa mara wanalenga na mashambulizi ya kundi la Taliban katika jimbo la Farah,kwenye paka na Iran,

.Kwa mujibu wa Rais Ashraf Ghani, askari na polisi 29 000 wameuawa katika vita katika ndani ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita.