PALESTINA. GAZA-HAKI

Gaza: Wanaume watano na mwanamke mmoja wahukumiwa kifo kwa kushirikiana na Israel

Picha ya Nasser Suleiman, Mkuu wa Mahakama za kijeshi katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linaloongozwa na Hamas, ilipigwa Mei 21, 2017
Picha ya Nasser Suleiman, Mkuu wa Mahakama za kijeshi katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linaloongozwa na Hamas, ilipigwa Mei 21, 2017 © AFP

Mahakama ya kijeshi ya Gaza imewahukumu kifo wanaume watano na mwanamke mmoja kwa "kushirikiana" na Israeli, mamlaka katika eneo hilo la Palestina linaloongozwa na kundi la Hamas imesema.

Matangazo ya kibiashara

Mwanamke huyo aliyehukumiwa kifo anaishi nchini Israeli na hakuwepo wakati wa kutolewa hukumu hiyo,kwa mujibu wa mamlaka huko Gaza.

Mahakama ilitoa jumla ya hukumu 14 kwa ushirikiano na Israeli, na watu nwengine nane wamehukumiwa kufanya kazi ngumu.

Mamlaka inawashtaki kuhusika katika mlipuko ambao uliua maafisa sita wa Hamas mwezi Mei 2018 na kundi la Hamas lilihusisha Israel kwa shambulizi hilo.

Mazingira ya mlipuko huo hayakuelezwa hadharani. Iyad al-Bozoum, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani huko Gaza, amesema kuwa shambulio hilo lilihusishwa na mfumo wa uhaini ulioendeshwa na Israel.

Israeli kwa upande mmoja, Hamas na washirika wake kwa upande mwingine walipigana vita tatu katika Ukanda wa Gaza tangu 2008.

Baada ya miezi kadhaa ya mvutano, pande hizo mbili ziliafikiana kusitisha mapigano tarehe 13 Novemba.