SAUDI ARABIA-MAREKANI-UCHUNGUZI

Maseneta nchini Marekani wamhusisha mwanamfalme Salman kwa mauaji ya Khashoggi

Capitol Washington, makao makuu ya Bunge la Seneti la Marekani.
Capitol Washington, makao makuu ya Bunge la Seneti la Marekani. ©REUTERS/Joshua Roberts

Maseneta nchini Marekani, baada ya kupewa taarifa ya kina na Mkurugenzi wa taasisi ya Ujasusi CIA, wanasema sasa wanaamini kuwa Mwanamlfalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman, aliagiza kuuawa kwa Mwanahabar Jamal Khashoogi.

Matangazo ya kibiashara

Aidha, wamesema wameshangazwa namna serikali ya Marekani ilivyoshughulikia mauaji ya Khashoogi, baada ya rais Donald Trump kuonekana kuutetea uongozi wa Saudi Arabia.

Seneta wa mwenye ushawishi mkubwa kutoka chama cha Republican Lindsey Graham amesema ana "imani ya hali ya juu" kuwa Mohammed bin Salman (MBS) alipanga njama ya kumuua Khashoggi.

Senata Lindsey Graham kutoka chama cha Republican amemwelezea Mohammed Bin Salman, kama mtu asiye na akili timamu.

Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2. Mwanahabari huyo alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme bin Salman.