YEMEN-USALAMA-MAZUNGUMZO

Mji wa Hodeida waendelea kukumbwa na mapigano

Vikosi vya serikali vikipiga kambi katika mji wa Hodeida Novemba 10, 2018.
Vikosi vya serikali vikipiga kambi katika mji wa Hodeida Novemba 10, 2018. Khaled Ziad / AFP

Mapigano yamezuka tena katika mji wa bandari wa Hodeida nchini Yemen licha ya kuanza kwa muda wa kusitishwa kwa mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi wa kundi la Houthi.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yameanza usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne kwenye bandari ya Hodeida, magharibi mwa nchi, licha ya mkataba wa kusitisha mapigano kati ya serikali na waasi wa Houthi kuanza kutumika, kwa mujibu wa chanzo kilo karibu na serikali.

Siku ya Alhamisi wiki iliopita wajumbe wa serikali na waasi wa kundi la Houthii walifikia makubaliano nchini Sweeden chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, na kuamua kusitisha mapigano.

Mapigano makali na mashambulizi ya anga yalikuwa yakiendelea mwishoni mwa wiki iliyopita.

Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF linasema mapigano haya mapya yanatatiza shughuli zao.