UTURUKI-MAREKANI-SYRIA-USALAMA

Uturuki yafutilia mbali onyo la Marekani

Rais wa Uturuki Tayyip Recep Erdogan (kushoto) na mwenzake wa Marekani Donald Trump, Jumanne Mei 16, 2017, katika ikulu ya White House.
Rais wa Uturuki Tayyip Recep Erdogan (kushoto) na mwenzake wa Marekani Donald Trump, Jumanne Mei 16, 2017, katika ikulu ya White House. REUTERS/Kevin Lamarque

Uturuki ina mpango wa kuendelea mapambano dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi baada ya vitisho vya Trump, kwa mujibu wa msemaji Erdogan. Taarifa ambayo imethibitishwa na chanzo cha serikali ya Uturuki

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili Rais wa Marekani Donald Trump aliionya Uturuki dhidi ya kile alichoita janga la kiuchumi ikiwa itashambulia Wakurdi baada ya kuondoka kwa askari wa Marekani nchini Syria.

Wakati huo huo Rais Trump alitolea wito Wakurdi "kutoichokoza" Ankara.

Marekani "itaiangamiza Uturuki kiuchumi ikiwa itafanya mashambulizi dhidi ya Wakurdi," alisemal Donald Trump, usiku wa Jumapili, Januari 13.

Urusi, Iran na Syria walikuwa wakinufaika zaidi katika sera ya muda mrefu ya Marekani ya kuangamiza kundi la Islamic State nchini Syria.

Rais Trump amesema "pia tunanufaika na hilo, lakini muda umewadia kuwarejesha nyumbani askari wetu. Vita visio kuwa na misho vikome, "Donald Trump ameongeza kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Tangazo la Desemba la kuondoa askari wa Marekani nchini Syria lilikaribishwa na Uturuki lakini lilizua wasiwasi mkubwa kwa upande wa wapiganaji wa Kikurdi ambao walisaidia Marekani katika vita dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametishia kuzindua shambulio la kijeshi kaskazini mwa Syria kuwatimua wapiganaji wa Kikurdi.