SYRIA-MAREKANI-IS-USALAMA

Kumi na sita waangamia katika shambulio Manbij, Syria

Picha ya eneo la shambulio la kujitoa muhanga, Manbij, Januari 16, 2019
Picha ya eneo la shambulio la kujitoa muhanga, Manbij, Januari 16, 2019 AFP / ANHA

Kundi la Islamic State limekiri kuwa lilihusika na shambulio la kujitoa muhanga lililoua watu 16 ikiwa ni pamoja na Wamarekani 4 katika mji wa Manbij, nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Kwa kushambulia Manbij, karibu na mpaka na Uturuki, mbali na ngome yake ya mwisho kusini mashariki mwa Deir Ezzor, kundi la Islamic State limeonyesha kuwa bado lina uwezo wa kufanya uharibifu.

Mshambuliaji ewa kujitoa muhanga alijilipua kwenye mgahawa maarifu ambao mara nyingi hutembelewa na askari kutoka wa muungano wa kimataifa, unaoongozwa na Marekani. Muda mfupi baada ya, tukio hilo, kundi la Islamic sate lilikiri kuhusika na shambulio hilo katika taarifa iliyopchapishwa na shirika lake la propaganda Ahmaq.

Kwa mujibu wa vymbo kadhaa nchini Syria, wanajeshi wanne wa Marekani wameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa kwenye mlipuko katika mji wa Manbij nchini Syria. Tovuti ya habari yenye mafungamano na kundi la Islamic State (IS), Ahmaq imetoa tangazo, ikisema mshambuliaji wa kujitoa muhanga amewalenga wanajeshi wa muungano unaoongozwa na Marekani walioko Manbij.

Msemaji wa Ikulu ya White House mjini Washington Sarah Sanders amesema Rais Donald Trump amearifiwa kuhusu shambulio hilo.

Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu nchini Syria (OSDH) lenye makao yake nchini Uingereza (OSDH), takribani watu saba wameuwawa na watu wengine tisa wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo.

Shambulio hilo limetokea wakati Marekani ikianza mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Syria, na kusafirisha vifaa vyao kutoka Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo na kuvipeleka nchini Iraq.