UAE-PAPA-USHIRIKIANO

Papa Francis kuendeleza mazungumzo ya kidini Abu Dhabi

Papa Francis na Imamu wa Msikiti wa Al-Azar Ahmed Mohamed el-Tayeb, Abu Dhabi, Februari 3, 2019.
Papa Francis na Imamu wa Msikiti wa Al-Azar Ahmed Mohamed el-Tayeb, Abu Dhabi, Februari 3, 2019. WAM/Handout via REUTERS

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis amewasili Abu Dhabi Jumapili, Februari 3 jioni. Anatarajia kuhudhiria Jumatatu wiki hii mkutano wa dini mbalimbali usiokuwa wa kawaida katika rasi ya Arabuni.

Matangazo ya kibiashara

Papa Francis anatarajia kushiriki misa JUmanne wiki hii ambapo takriban watu 120,000 wanatarajiwa kuhudhuria.

Ziara hii ya Papa katika Umoja wa Falme za Kiarabu UAE ni ya kihistoria.

Papa Francis amewasili katika Umoja wa falme za kiarabu kwa ziara ya kwanza kuwahi kufanyika na kiongozi mkuu katika kanisa Katoliki huko Arabuni.

Umoja wa Falme za kiarabu unahusika katika mzozo nchini Yemen kama sehemu ya muungano unaoongozwa na Saudia.

Kabla ya kuondoka alielezea wasiwasi wake kuhusu vita nchini Yemen.

Haijulikani wazi iwapo atazungumzia suala hilo mbele ya umma au katika faragha wakati wa ziara yake.

Siku ya Alhamisi wiki jana Papa alitoa heshima zake kwa Umoja huo wa flame za Kiarabu kuwa "nchi ambayo inajaribu kuwa mfano wa watu kuishi pamoja, mfano wa udugu, na eneo lililo na raia wa tabaka na tamaduni mbali mbali ".