UAE-PAPA-USHIRIKIANO

Kiongozi wa kanisa Katoliki ahitimisha ziara yake Arabuni

Papa Francis na Imam Mkuu wa Al-Azhar, Sheikh Ahmed al-Tayeb wakitia saini kwenye hati kuhusu vita dhidi ya ubaguzi, wakati wa mkutano kidini, Februari 4, 2019.
Papa Francis na Imam Mkuu wa Al-Azhar, Sheikh Ahmed al-Tayeb wakitia saini kwenye hati kuhusu vita dhidi ya ubaguzi, wakati wa mkutano kidini, Februari 4, 2019. REUTERS/Tony Gentile

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis anahitimisha ziara yake ya kihistoria katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na anatarajia kuongoza misa waumini wa kanisa Katoliki nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Papa Francis amepongeza Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kutokuwa na ubaguzi wa kidini na kusem akuwa nchi hiyo inatakiwa kuwa mfano kwa mataifa mengine yenye ubaguzi wa kidini.

Pia amekaribisha juhudi za Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kuwapa ajira wahamiaji ambao wengi wao ni kutoka Ufilipino na India.

Jorge Bergoglio, ambaye mwenyewe ni mtoto wa wahamiaji aliyeishi kwa muda mrefu nchini Argentina, nchi yenye tamaduni mbalimbali, huwa anakerwa na matatizo yanayowakabili raia waliotoroka nchi zao.

Umoja wa Falme za Kiarabu una wakazi zaidi ya 85% ya wahamiaji. Raia kutoka nchi za Asia ni asilimia 65 ya wakaazi wa nchi hiyo na wameajiriwa katika sekta zote, kuanzia ujenzi hadi katika hoteli.

Takribani Wakatoliki milioni moja wanaishi katika Umoja wa Falme za Kiarabu, sawa na mkaazi mmoja kati ya kumi. Umoja wa Falme za Kiarabu una makanisa nanae ya Katoliki, idadi kubwa ya makanisa Katoliki katika kanda hiyo.

Mabasi zaidi ya 2,000 yanatarajia leo Jumanne kusafirisha waumini kutoka nchini kote kwenda Abu Dhabi kushiriki misa itakayoongzwa na Papa Francis.